Southampton imemtangaza Nathan Jones kuwa kocha wao mkuu akirithi nafasi ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Ralph Hasenhuttl huku kocha huyo akisema kuwa ilikuwa ndoto yake kuwa meneja wa Ligi kuu ya Uingereza.

 

Southampton Yamtangaza Jones Kama Mbadala wa Hasenhuttl

Jones ni raia wa Wales, ambaye ana miaka  49, na maepewa mkataba wa kudumu na klabu hiyo hadi 2026 akiwa amebadilisha maisha yake katika klabu ya Championship ya Luton kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu huko St Mary’s.

Southampton wanasema kuwa kazi yake ya kwanza itakuwa kuwaelekeza Watakatifu hao wanaopitia wakati mgumu baada ya kuwa katika nafasi mbaya kwenye msimamo na anatarajiwa abadilishe mwenendo wa timu hiyo.

Jones alisema: “Ninajivunia sana kupewa nafasi hii. Ninajua mengi kuhusu klabu tangu zamani za The Dell, hadi kuja hapa St Mary’s, na ni klabu nzuri ya kandanda, familia yangu wengi ni mashabiki wa Southampton, na ninajisikia fahari sana kupewa nafasi hiyo”

Southampton Yamtangaza Jones Kama Mbadala wa Hasenhuttl

Jones alitumia miaka mitano na nusu katika vipindi viwili kwenye dimba la Luton akiiongoza klabu ya Bedfordshire hadi nusu fainali ya mchujo ya Ubingwa msimu uliopita. Kocha huyo anachukua mikoba ya St Mary’s huku Saints wakiwa nafasi ya 18 kwenye Ligi ya Primia kufuatia msululu wa vipigo sita kutoka kwenye mechi 6.

Mechi inayofuata ya Southampton itakuwa ni dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi na itakuwa ni mechi ya kwanza ya Jones kabla ya mapumziko ya Kombe la Dunia.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa