Klabu ya Inter Milan imefanikiwa kupata ushindi wa kishindo baada ya kuifunga klabu ya Bologna kwa jumla ya mabao sita kwa moja wakiwa katika dimba lao la nymbani. Hii imekuja baada ya kupoteza mchezo uliomalizika wikiendi iliyomalizika.

Baada ya kupoteza dhidi ya klabu ya Juventus wikiendi iliyoisha klabu hiyo imefanikiwa kupata matokeo mazuri dhidi ya klabu ya Bologna na ukiwa ni ushindi mnono kabisa usiku wa jana katika mchezo wa ligi kuu nchini Italia Serie A.inter milanMabao ya Edin Dzeko,Lautaro Martinez,Robin Gossens,Hakan Calhanoglu na magoli mawili ya Federico Dimarco yaliiwezesha Inter Milan kupata ushindi mnono katika mchzo huo na klabu hiyo kuweza kupata alama tatu na kufikisha jumla ya alama 27 kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Kocha wa klabu ya Inter Milan ametumia mchezo huo kama sehemu ya kuomba radhi kutokana na matokeo mabaya waliyoyapata wikiendi iliomalizika dhidi ya klabu ya Juventus katika Derby ya Italia.inter milanKlabu ya Inter Milan itacheza mchezo wake wa mwisho kabla ya mapumziko ya kombe la dunia siku ya jumapili dhidi ya klabu ya Atalanta ambao unatazamiwa kua mchezo mgumu kwa vijana hao wa Simeone Inzaghi.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa