Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Deschamps amesema kuwa mshambuliaji wake Karim Benzema atafanya kila awezalo kuwa sawa kwa 100% kwa Kombe la Dunia baada ya kujumuishwa katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya michuano hiyo huku akiwa na msimu wa majeraha.

 

Deschamps: "Benzema Anafanya Kila Kitu Kuwa Sawa kwa 100%"

Benzema alishinda tuzo yake ya kwanza ya Ballon d’Or baada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa ubingwa wa LaLiga na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufunga mabao 44 muhula uliopita lakini amevumilia kampeni ya kufadhaisha ya 2022-23 hadi sasa.

Mshambuliaji huyo ameanza mechi 11 pekee katika mashindano yote msimu huu, akifunga mabao sita na kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 alikuwa anasumbuliwa na uchovu wa misuli.

Hata hivyo, Benzema ataungana na makinda Kylian Mbappe, Antoine Griezmann na Olivier Giroud miongoni mwa washambuliaji wa Ufaransa huko Qatar na Deschamps anatumai atakuwa katika hali ya juu zaidi.

Deschamps: "Benzema Anafanya Kila Kitu Kuwa Sawa kwa 100%"

Deschamps amesema kuwa; “Benzema amekuwa na majeraha machache lakini anajua kuwa Kombe la Dunia ni wakati muhimu sana”. Kocha huyo ameyasema hayo baada ya kutoa kikosi chake hapo jana cha wachezaji 25.

Beki wa Manchester United Raphael Varane pia amejumuishwa licha ya kupata jeraha la mguu katika sare ya Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea mwezi uliopita na Deschamps ana matumaini kuhusu uwezekano wake wa kumenyana na Australia katika mechi ya ufunguzi ya Kundi D mnamo Novemba 22.

Kocha huyo ameongezea kuwa Presnel Kimpembe alikuwa na tatizo kidogo lakini atakuwepo kwa mechi ya mwisho ya Ligi ya Jumapili ambapo PSG watakuwa wakimenyana dhidi ya Auxerre.

Deschamps: "Benzema Anafanya Kila Kitu Kuwa Sawa kwa 100%"

Washindi hao wa Kombe la Dunia wataelekea Qatar wakiwa na safu ya kiungo iliyopungua baada ya Paul Pogba na N’Golo Kante kuondolewa, huku mabeki wa kushoto Ferland Mendy na Lucas Digne, pamoja na kipa wa Milan Mike Maignan  ambaye alipata jeraha la mguu mnamo Septemba wakiwa ni miongoni mwa ambao hawatakuepo.

Ufaransa watakuwa na nahodha wao ambaye ni kipa wa Tottenham, Hugo Lloris nchini Qatar, ambaye kujumuishwa kwake katika kikosi cha nne cha Kombe la Dunia kunamfanya kuwa sawa na rekodi ya Kitaifa iliyowekwa na Thierry Henry katika mashindano ya 1998, 2002, 2006 na 2010.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa