Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone ameitaka timu hiyo kurejea kwenye kiwango chao baada ya Kombe la Dunia kwa nia ya kubadili msimu wao unaoyumba kufuatia kuangusha pointi kwenye michezo yao.

 

Simeone Aitaka Atletico Ibadili Msimu Baada ya Kombe la Dunia

Atletico walichapwa 1-0 ugenini dhidi ya  Mallorca siku hapo jana na kuendeleza mwendo wao wa kutoshinda hadi mechi tano katika michuano yote, na  hawajawahi kustahimili mfululizo mbaya zaidi wakati wa uongozi wa Simeone.

Mechi inayofuata itakuwa ni ya Copa del Rey siku ya Jumamosi watakayocheza dhidi ya SD Almazan wakiwa ugenini na hapo hawatacheza mchezo woowte mpaka pale Kombe la Dunia litakapomalizika.

Kichapo cha Jumatano kinaiacha Atletico nafasi ya sita kwenye LaLiga, ingawa ushindi mkubwa kwa Rayo Vallecano dhidi ya Celta Vigo Alhamisi unaweza kuwashusha vijana hao wa Simeone.

Simeone Aitaka Atletico Ibadili Msimu Baada ya Kombe la Dunia

Simeone aliambia DAZN kuwa; “Kusitishwa kwa mchuano kutaleta amani ya akili kufanya kazi, na kuwaokoa kikamilifu wachezaji waliojeruhiwa, ambao kwa hakika tunawahitaji, na natumai kuwa baada ya Kombe la Dunia watarejea na wazo la kubadilisha hali hii ngumu.”

Kocha huo alisema kuwa kusema kuwa wamekosa nguvu katika michezo yote ni kisingizio rahisi sana kwani wanafanya makosa mengi katika safu ya ulinzi ambayo inafanya michezo kuwa vita zaidi kwao.

Simeone Aitaka Atletico Ibadili Msimu Baada ya Kombe la Dunia

Anasema kuwa uhalisia unawafanya waondoke na kichapo ambacho kinauma na ni wazi kinawafanya wafanye kazi kwa bidii katika muda wanaoupata, kwasababu Laliga ikirejea kutakuwa na michezo migumu.


AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa