Diego Simeone: Isingwezekana Ronaldo Kucheza Atletico.

Kocha wa klabu ya Atletico Madrid Diego Simeone amefunguka kuhusiana na tetesi zilizokua zikimuhusisha staa wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo kujiunga na klabu yake majira ya joto yaliyopita.

Atletico Madrid walikua miongoni mwa vilabu vilivyohusishwa staa huyo kuhamia majira ya joto pamoja na vilabu vya Bayern Munich,Chelsea, Napoli ambapo staa huyo ilisemekana anahitaji klabu ambayo inashiriki ligi ya mabingwa ulaya wakati amabpo Manchester United ilishindwa kufuzu michuano hiyo.diego simeoneKocha huyo aliweka wazi kua mchezaji huyo asingeweza kujiunga na klabu hiyuo kutokana na mahusiano yake na klabu ya Real Madrid na wakati huo klabu hizo mbili ni mahasimu wakubwa jambo ambalo Diego Simeone hakuona likitokea.

“Kile ambacho kilizungumzwa na waandishi wa habari Sio kitu kilichotokea, Watu muda mwingine huzungumza ili kukuambia tu kile wanachotaka kukuambia, Sio kile kinachotokea Ronaldo ni Nembo ya Real Madrid” Simeone Alizungumza.

“Hungemwona Martin Palermo, Juan Roman Riquelme wakichezea River plate, Au Ariel Ortega akichezea Boca Juniors. Kuna hali fulani ziko wazi kabisa” Alisema Diego Simeone akieleza ugumu wa mchezaji huyo kuichezea Atletico Madrid.diego simeoneKocha huyo ametolea mifano kwa wachezaji wa timu mahasimu duniani kama Boca Junior na River plate kutoka Argentina timu hizo zenye uhasama mkubwa hivo ni ngumu kwa mchezaji kutoka klabu moja kuichezea nyingine kati ya hizo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.