Simba Yatinga Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Klabu ya Soka ya Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya kigi ya mabingwa Afrika baada ya kuitoa klabu ya Primero de Agosto ya nchini Angola.

simbaKlabu hiyo imefanikiwa kufuzu hatua hiyo baada ya kucheza mechi nne mbili za hatua ya awali dhidi ya klabu ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika michezo miwili iliyopigwa nchini Malawi na hapa nchini Tanzania huku Mnyama akishinda michezo yote.

Katika hatua ya kwanza Simba wamefanikiwa kuwafunga Premero de Agosto kwenye michezo miwili pia kama ambavyo walifanya dhidi ya Nyasa ya Malawi baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyomalizika nchini Angola na Simba kushinda mabao matatu kwa moja leo walifanikiwa kushinda bao moja kwa bila kupitia Moses Phiri na kumfanya mnyama kwenda hatua ya makundi Afrika.

Mnyama ambaye alishindwa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika msimu uliomalizika baada ya kufungwa nyumbani na klabu ya Jwaneng Galaxy kutoka Bostwana lakini kosa hilo hawakulirudia leo hii baada ya kuhakikisha wanashinda na kufuzu hatua hiyo kibabe.simbaKlabu hiyo kwasasa inakua klabu ya pili kutaka ukanda wa Afrika mashariki kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya jana klabu ya Vipers kutoka nchini Uganda kufanya hivo.

Acha ujumbe