Kocha mkuu wa Juventus Massimiliano Allegri alimtoa Paul Pogba kwenye mipango yake ya Juventus kwa mechi ya Ijumaa dhidi ya Empoli huku akisema itakuwa wazimu mtupu kuharakisha kumpanga kikosini hapo kabla hajapona.

Juventus wameshindwa kumchezesha Pogba au Federico Chiesa msimu huu, huku kiungo huyo wa kati wa Ufaransa akifanyiwa upasuaji wa goti mwezi uliopita na mshambuliaji wa Italia Chiesa akiuguza jeraha lake alilolipata mwezi Januari.
Hapo awali Pogba alikuwa na wasiwasi wa kukosa Kombe la Dunia lijalo nchini Qatar, ingawa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps alikuwa na furaha kuhusu kupona kwake mapema wiki hii.
Akizungumza katika hafla ya Jumatatu ya tuzo ya Ballon d’Or, Deschamps alisema: “Programu yake inaendelea vizuri. Muhimu ni kwamba amepona nadhani atakuwa na hali ya utayari ambapo ni jambo zuri”

Licha ya Pogba na Chiesa kupigwa picha kwenye mazoezi ya timu hivi karibuni, kocha mkuu Allegri alisema Juventus lazima iwachukulie kwa tahadhari wachezaji wao waliorejea huku akisema kuwa ukweli ni kwamba Chiesa na Pogba ni muhimu kikosini.
Allegri amesema kuwa Chiesa tayari ameshapiga hatua na Jumamosi asubuhi watakuwa na mechi ya kirafiki kwa Federico, kuangalia namna ambayo anavyofanya uwanjani. Kwa Pogba amefanya baadhi ya kazi na timu, lakini wapo Alhamisi hadi Jumanne kuna siku nne za kujiandaa.
Baada ya kukutana na Empoli, Juventus watakuwa na siku tatu tu za kujirekebisha kabla ya mchuano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica, lakini Allegri asingevutiwa na iwapo mshambuliaji Dusan Vlahovic atapumzishwa Ijumaa.

Vlahovic amefunga mabao matatu katika mechi tatu za Serie A dhidi ya Empoli, ikiwa ni pamoja na mara mbili yake ya kwanza ya ligi akiwa na Juventus mwezi Februari. Mserbia huyo pia ametikisa nyavu mara tano katika mechi tano za ligi ya nyumbani msimu huu.

