Allegri Anaamini Kuifunga Benfica Baada ya Ushindi Mkubwa wa Jana.

Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ameiunga mkono timu yake hapo jana kwenye ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Empoli huku akiamini vyema kuwa timu yake itafanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica baada ya kuwa na kiwango bora hapo jana.

 

Allegri Anaamini Kuifunga Benfica Baada ya Ushindi Mkubwa wa Jana.

Juventus  walifuatia ushindi wao wa Dabi  dhidi ya Torino wikendi iliyopita kwa kuonyesha kiwango cha kuvutia kwenye Uwanja wa Allianz Arena, ambapo Moise Kean aliwaweka mbele kwa bao lake la kwanza tangu Aprili.

Kibarua cha  Allegri kilikuwa hatarini kutokana na matokeo mabovu aliyokuwa akiyapata baada ya kupata kichapo kutoka kwa AC Milan, Maccabi Haifa lakini wababe hao wa Turin wameonekana kubadili gia na kuanza kugawa vichapo.

Allegri amesema kuwa ni lazima washinde mchezo wao dhidi ya Benfica ya Ureno siku ya Jumanne ili waweze kupata nafasi ya kufuzu kwa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwani wasipofuzu michuano hiyo wataangukia michuano ya Uropa.

Allegri Anaamini Kuifunga Benfica Baada ya Ushindi Mkubwa wa Jana.

Kocha anasema; “Kwa bahati mbaya inabidi tukimbizane na ubingwa kwa pointi zilizopotea dhidi ya Salernitana na Monza. Jumanne itakuwa mechi muhimu kwa sababu mbili, hatuko nje ya Ligi ya Mabingwa na hata hatuko kwenye Ligi ya Uropa.

Juventus wanakutana na timu yenye nguvu, na wanaweza kwenda huko na kupoindua meza walifungwa nyumbani na Banfica wanahitaji kujiamini huku akifurahishwa na uchezaji wa mshambuliaji Kean na kiungo wake Rabiot na amesema kuna mengi zaidi kutoka kwa wawili hao.

Hakuishia hapo alizidi kuwasifia wachezaji hao na kusema kuwa Kean alifanya vizuri dhidi ya Torino na akakosa bao, angeweza kufunga zaidi ya bao moja usiku wa leo haswa kipindi cha kwanza kwani alicheza vizuri kiufundi. Wakati Rabiot amekua sana anacheza michezo muhimu kwahiyo anadhani bado ana nafasi kubwa ya kuboresha kiwango chake.

Allegri Anaamini Kuifunga Benfica Baada ya Ushindi Mkubwa wa Jana.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.