Conte: Kulusevski Anaweza Asirejee Kabla ya Kombe la Dunia

Kocha mkuu wa Spurs Antonio Conte ana wasiwasi kwamba mchezaji wake Dejan Kulusevski huenda asicheze Tottenham kabla ya Kombe la Dunia baada ya winga huyo kupata shida katika kupona jeraha la misuli ya paja.

 

Conte: Kulusevski Anaweza Asirejee Kabla ya Kombe la Dunia

Kulusevski hajashiriki katika kikosi cha Spurs tangu mwezi uliopita walipoicharaza Leicester City mabao  6-2, baada ya kupata jeraha hilo akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa  Uswidi  ambao walishindwa kufuzu kwa michuano hiyo nchini Qatar.

Ingawa awali uchezaji wa Richarlison uliiruhusu Spurs kukabiliana na kukosekana kwa Kulusevski, Richarlison ambae ni mshambuliaji wa Brazil alishindwa kuendelea na mchezo ambao walikuwa wakicheza dhidi ya Everton walishinda kwa mabao 2-0, na hivyo kumuacha Conte akikosa chaguo la mshambuliaji.

Akizungumza kabla ya mechi ya Jumapili dhidi ya Newcastle United, Conte aliongea kuhusu Kulusevski na kusema kuwa: “Nadhani tunapaswa kusubiri muda kidogo kumuona pamoja nasi, ni vivyo hivyo kwa Richarlison, na kwahakika hali ya aina hiyo huleta ugumu mkubwa.

Conte: Kulusevski Anaweza Asirejee Kabla ya Kombe la Dunia

Kwasasa Conte amebaki na Harry Kane na Son Heung-Min ambao wana afya njema na anatumaini wataendelea kubaki hivyo au itabidi afikirie kuvaa viatu vyake acheze. Alisema kuwa unapoenda kucheza Ligi ya Mabingwa, haswa ikiwa unacheza ligi kuu, lazima ujue kuwa utakuwa na msimu mgumu wa majeruhi kwa michezo mikubwa kwani  wachezaji wanachoka.

Tottenham wamepoteza michezo miwili kati ya minne iliyopita ya Ligi Kuu ya Uingereza wakikumbana na vipigo vingi katika kipindi hicho kama walivyopoteza katika mechi 21 zilizopita kwenye shindano hilo.

Conte: Kulusevski Anaweza Asirejee Kabla ya Kombe la Dunia

Matokeo ya Jumatano ya 2-0 dhidi ya Manchester United yaliwakilisha mara ya kwanza kwa Spurs kushindwa kufunga katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu, na kumfanya Conte kutangaza kuwa timu hizo mbili zilikuwa zikifanya kazi kwa “ngazi tofauti”.

Hakusita kuongelea kuhusu dirisha la usajili lijalo na kusema kuwa klabu itatathmini chaguo lao wakati wa mapumziko ya Kombe la Dunia.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.