Imethibitishwa kuwa Mwenyekiti wa klabu ya Juventus inayoongozwa na kocha mkuu Massimiliano Allegri, Andrea Agnelli na bodi nzima ya klabu hiyo wamejiuzulu ghafla.

Juventus itapata mabadiliko makubwa katika usimamizi baada ya kuthibitishwa kuwa mkutano wa wanahisa uliopangwa kufanyika wiki iliyopita umeahirishwa hadi mwezi ujao, huku Kando na Agnelli amabye amekuwa akiiongoza klabu hiyo tangu 2010, makamu wa rais Pavel Nedved na mkurugenzi mkuu Maurizio Arrivabene pia ni miongoni mwa walioacha kazi.
Arrivabene atasalia kuwa afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo kusimamia kuanzishwa kwa bodi mpya, ambayo itathibitishwa Januari.
Kujiuzulu kwa pamoja kunakuja baada ya taarifa za kifedha za Juventus kuchunguzwa na waendesha mashtaka na mdhibiti wa soko wa Italia Consob katika miezi ya hivi karibuni kwa madai ya uhasibu wa uwongo na udukuzi wa soko.

Katika taarifa kutoka kwa klabu hiyo, Juventus ilithibitisha uamuzi wa bodi ya kujiuzulu umekuja kufuatia ushauri uliotolewa na Consob na mkaguzi wa hesabu Deloitte ikisema kuwa;
“Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, kwa kuzingatia umuhimu wa masuala ya kisheria na kiufundi ya uhasibu yanayosubiri, wameona ni kwa manufaa ya kijamii kupendekeza Juventus kupitisha Bodi mpya ya Wakurugenzi kushughulikia masuala haya”, ilisoma kuwa;
“Kufikia hili, kwa pendekezo la mwenyekiti Andrea Agnelli, wajumbe wote wa Bodi ya Wakurugenzi waliohudhuria mkutano huo walitangaza kwamba walijiuzulu, bodi imemtaka Maurizio Arrivabene kushikilia nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu.”

Tangazo hilo linaonekana kumaliza uhusiano wa miongo na klabu kwa Agnelli, ambaye alikuwa mwanachama wa nne wa familia yake kuhudumu kama mwenyekiti.
Juventus kwa sasa wako nafasi ya tatu kwenye Serie A, lakini walikosa kufuzu kwa raundi ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa, badala yake wakadondokea kwenye Ligi ya Europa msimu huu.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


