Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa Andrien Rabiot amezungumza kuhusu hatma yake ndani ya klabu ya Juventus ambaye anaitumikia mchezaji huyo kwasasa.

Kiungo huyo ambaye kwasasa anaitumikia timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar na akionekana kama nguzo muhimu kwenye kikosi cha timu hiyo chini ya kocha Deschanmps.rabiotKwenye mchezo wa kwanza wa timu ya taifa ya Ufaransa ambao wameshinda magoli manne kwa moha huku Rabiot akifanikiwa kufunga bao moja na kutengeneza bao lingine hivo akiwa amehusika kwenye mabao mawili katika mchezo huo.

Kiungo huyo ambaye alikua anahusishwa kuhamia klabu ya Manchester United mwishoni mwa dirisha la usajili uliopita na dili kushindwa kukamilika siku za mwishoni kitu kilichomfanya nyota huyo kusalia kwenye viunga vya Turin.

Kiungo Andrien Rabiot amesema sio wakati wa kuzungumzia hatma yake ndani ya klabu ya Juventus ambapo unamalizika mwishoni mwa msimu wa mwaka 2023 huku akisema hajui kama ataweza kubakia kwenye miamba hiyo ya Juventus au kuondoka klabuni hapo.rabiotKiungo huyo amesema kiwango chake cha hivi karibuni kinaweza kuwavutia Juventus kumuongezea mkataba au kuvutia vilabu vingine pia vitakavyohitaji huduma yake kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa