Kiungo wa Yanga Zawadi Mauya ameanza kwenye kikosi cha kwanza hii leo ambacho kitaenda kumenyana dhidi ya washika mkia wa Ligi kuu ya NBC Ihefu, baada ya kutoka kushinda mechi yao iliyopita.

Zawadi ameingia hii leo kuchukua nafasi ya Gael Bigirimana ambaye amekuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi hicho kinachoongozwa na kocha Nasredine Nabi.
Lakini kwa upande wa Ihefu wao watamkosa Obrey Chirwa licha ya Jumma Nyoso kurejea kikosini lakini bado matumaini ni asilimia chache sana kwa kikosi cha Ihefu kupata ushindi.
Yanga endapo itashinda mchezo wao hii leo, itafikisha mechi 50 “Unbeaten” huku wakizidi kuongoza ligi wakiwa kileleni kwenye msimamo baada ya kufululza kupata matokeo ya kuvutia.

Kinara wa mabao NBC Primia Ligi Fiston Kalala Mayele ameanza kwenye kikosi akitarajia kubeba kiatu cha dhahabu msimu utakapomalizika baada ya kufikisha mabao 10 hadi sasa.
Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.
BONYEZA HAPA KUCHEZA


