Simba Yadondosha Alama Kaitaba

Baada ya ushindi mnono kabisa walioupata mechi iliyopita, Simba jana wameshindwa kutwaa pointi tatu katika uwanja wa Kaitaba walipokuwa wakimenyana dhidi ya Kagera Sugar ya Mecky Mexime.

 

Simba Yadondosha Alama Kaitaba

Simba walitanguliwa kufungwa bao mapema kabisa na mchezaji wa Kagera Sugar Deus Bukenya, kabla ya Henock Inonga kuja kuswazisha bao hilo katika dakika ya 38 ya mchezo kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili waliporejea licha ya Wekundu wa Msimbazi kufanya majaribio ya hatari ya kupata bao lakini milango ikawa migumu kufunguka kwa upande wao kwani vijana wa Kaitaba waliweza kulinda lango lao.

Simba Yadondosha Alama Kaitaba

Hivyo Wekundu wa Msimbazi mpaka sasa wanafikisha sare 5 katika michezo yake 17 ambayo amecheza hadi sasa na akiwa nyuma ya pointi 6 kwa kinara wa Ligi Yanga ambaye ana alama zake 44 hadi sasa.

Mchezo unaofata wa vijana wa Mgunda watamenyana dhidi ya KMC tarehe 26 siku ya Jumatatu huku mechi ya kwanza walitoshana nguvu. Kagera wao watakipiga dhidi ya Geita Gold tarehe 25.

Simba Yadondosha Alama Kaitaba

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.