Simba Yamnyatia Kelvin Nashon

Klabu ya Soka ya Simba imeanza mazungumzo na nyota wa klabu ya Geita Gold Kelvin Nashon Naftal ili aweze kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi.

Klabu ya Simba imepanga kuingia sokoni kipindi hichi cha dirisha dogo ili kuweza kukiboresha kikosi chake kuelekea michuano mbalimbali ambayo ipo mbele yao msimu huu, Na miongonimwa majina yanayotajwa kuhitajika na wekundu hao wa msimbazi ni kiungo huyo wa klabu ya Geita Gold.simbaTaarifa zinasema kua wekundu wa msimbazi inaelezwa kua wamempa ofa kiungo huyo mkataba wa miaka mitatu na mshahara mzuri, Huku kiungo huyo akiwa amebakiza mkataba wa miezi sita klabuni hapo ambalo suala hilo Simba wapo tayari kulipa fidia ya mkataba.

Kiungo Kelvin Nashon Naftal ambaye amewahi kutumikia timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 17 Serengeti Boys amekua akifanya vizuri tangu ajiunge na klabu hiyo ambayo imepanda daraja msimu uliomalizika.simbaKlabu ya soka ya Simba imekua kwenye mchakato mzito kuhakikisha wanarudisha ubingwa wao waliouopoteza mbele ya mahasimu wao klabu ya Yanga msimu uliomalizika, Na moja mikakati hiyo ni kuhakikisha wanaboresha kikosi chao kua imara zaidi kwajili ya kutetea taji lao.

Acha ujumbe