Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda amesema kuwa bado wapo kwenye mbio za ubingwa mpaka kufikia mwisho wa msimu.
Simba kwa sasa inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa wamekusanya pointi 41 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 47.

Akizungumzia mbio zao za ubingwa, Mgunda amesema “Tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata pointi saba kati ya tisa kwenye michezo mitatu ya ugenini.
“Kila timu ina ushindani kutokana na malengo waliyojiwekea kwenye ligi kwahiyo nategemea mechi ya tarehe 30 itakuwa ni ngumu na yenye ushindani mkubwa.

“Ligi hii ni kama mbio za riadha kuna anayeongoza na anayeshinda subiri itakapofika mwisho ndio tutajua nani mshindi, mimi naamini tupo kwenye mbio za ubingwa hivyo tusubiri mpaka mwisho tuone itakavyokuwa.”

