Kocha mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amewashutumu Brentford kwa “kunyoosha sheria” baada ya Liverpool kupata kichapo cha kushangaza cha 3-1 dhidi ya Bees hapo jana.

Bao la kujifunga la Ibrahim Konate na la kichwa la Yoane Wissa liliiweka Liverpool chini katika kipindi cha kwanza, huku kikosi cha Klopp kikipambana kustahimili matokeo ya Brentford.
Liverpool walifanya mabadiliko matatu wakati wa mapumziko ikiwa ni pamoja na Virgil van Dijk akitoka na mabadiliko hayo yalionekana kuwapa Wekundu hao matumaini wakati Alex Oxlade-Chamberlain aliporudisha bao katika mechi yake ya 100 ya Ligi Kuu ya Uingereza kwa klabu.
Hata hivyo, Bryan Mbeumo aliongeza bao lingine kwa nyuki baada ya kumuangusha beki wa Majogoo Konate mpira kabla ya kuuwahi mpira na kuipa Brentford ushindi wao wa kwanza dhidi ya Liverpool tangu 1938.

Kloop amesema kuwa; “Sina uhakika unaweza kudhibiti kila wakati kwa sababu kila kona ni tishio kubwa. Wananyoosha sheria katika wakati huu na mguso kamili wa mwili. Ulikuwa mchezo walioutaka kuliko ule tuliotaka. Waliweza kuuamuru kwa sababu ya jinsi ulivyopulizwa.”
Darwin Nunez alikosa nafasi nzuri ya kuipa Liverpool bao la kuongoza mapema, akimzunguka David Raya na kunyimwa lango na Ben Mee kwenye mstari wa goli. Hakuna mchezaji aliyepoteza nafasi kubwa zaidi kwenye Primia Ligi msimu huu kuliko Nunez 15.

Klopp alilalamikia ubadhirifu wa timu yake mbele ya lango, na kuongeza kuwa wanaruhusu bao la kwanza wakati wanapaswa kuwa mbele kwa mabao 2-0, wakiwa na nafasi kubwa za mabao kutoka kwa Darwin na Kostas Tsimikas. Darwin Nunez hatarajii Ben Mee kuteleza hapo.

