Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp mipango yake ni kuhakikisha anamaliza nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Na hiyo ni baada ya ushindi dhidi ya Aston Vila siku ya jumatatu.
Klabu ya Liverpool imefanikiwa kupunguza pengo la alama mpaka kufikia tano baina yao na Tottenham ambao wapo nafasi ya nne, Klabu hiyo ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ikiwa na alama 25 huku Tottenham wakiwa na alama 30.
Kocha Jurgen Klopp amekiri pengo la alama 15 baina yao na vinara wa wa ligi hiyo klabu ya Arsenal ni kubwa na halizuiliki, Hivo mipango yao ni kumaliza nafasi nne za juu ambapo wanaona pengo lililopo baina yao na nafasi ya nne sio kubwa sana na linaweza kufikika.
Klabu ya Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp haijawahi kumaliza nje ya nne bora kwa misimu sita ya kocha huyo, Hivo kocha ana kazi ya kuhakikisha hataharibu rekodi aliyoiweka katika klabu hiyo yenye maskani yake jijini Liverpool.
Kocha Jurgen Klopp anasema hawakuanza msimu vizuri lakini wanapaswa kukimbizana ili kuweza kufanya vizuri kwa msimu uliobakia, Kocha huyo anakiri kuzikamata timu zilizopo nafasi nne za juu ni ngumu kama watashinda michezo yao iliobakia lakini aliopo nafasi ya nne ana imani wanaweza kumkamata.

