Jurgen Klopp Ataka Firmino Asaini Mkataba Mpya

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amesema ana matumaini kua mshambuliaji wake raia wa Brazil Roberto Firmino atasalia kwenye viunga vya Anfield.

Kocha huyo anaamini nyota huyo anaweza kusalia klabuni hapo kwani klabu ya Liverpool ipo kwenye mazungumzo na Roberto Firmino ili kuangalia uwezekano wa kumuongezea mchezaji huyo mkataba mpya ili aendelee kusalia klabuni hapo.jurgen kloppKocha Jurgen Klopp anaamini kua Roberto Firmino bado ni mchezaji muhimu sana kwenye kikosi chake licha ya kusajili wachezaji tofauti tofauti, Lakini bado anaona mshamnbuliaji huyo ni muhimu kwenye timu yake.

Roberto Firmino ni miongoni mwa wachezaji wa Liverpool waliocheza kwenye klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kushinda kila taji, Huku na yeye akiwa miongoni mwa mchezaji aliechangia mafanikio hayo kwa kiwango kikubwa.jurgen kloppKlabu ya Liverpool inaelezwa kwasasa imeanza majadiliano na wakala wa mchezaji huyo ili kumpa mkataba mpya, Jambo ambalo linamfanya Jurgen Klopp kuamini mshambuliaji wake Roberto Firmino ataendelea kusalia klabuni hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.