Hatimaye Bingwa wa Mapinduzi Cup amepatikana hapo jana na si mwingine bali ni Mlandege FC ambaye amechukua Kombe hilo baada ya kumcharaza Singida Big Stars kwa mabao 2-1.

Mlandege amejidhatiti na kuweza kulibakiza Kombe hilo nyumbani kwao huku kipindi cha kwanza pekee kikitosha kuwapa Ubingwa timu hiyo ya visiwani Zanzibar ambapo kabla ya dakika 45 kumalizika walikuwa wamekwisha tupia mabao mawili.
Baada ya kurejea kwa kipindi cha pili vijana wa Pluijm walifunga bao la kwanza ambalo halikutosha kuwapa matumaini ya kubeab kombe hilo kwa mara ya kwanza, na mpaka kipyenga cha mwamuzi kinamalizika timu hiyo ilikuwa tayari imeumaliza mwendo.

Mlandege mpaka anaingia fainali ameweza kumfunga Simba ambaye ndiye alikuwa bingwa mtetezi, akaja akamfunga Namungo na sasa amemfunga Singida kwenye fainali na hatimaye kutangazwa kuwa ni mabingwa wapya wa Kombe hili.
Mfungaji bora wa michuano hii ni Francy Kazadi, Mchezaji bora Chipukizi Said Mussa Said, Golikipa bora ni Mperule, Mchezaji Bora Yusuf Kagoma.

