Kiungo mshambuliaji wa Yanga raia wa Ghana, Bernard Morrison, amerejea kikosini baada ya kutatua matatizo yake na uongozi pamoja na benchi la Ufundi chini ya Kocha Nasreddine Nabi.

Morrison ambaye ametakiwa kutofanya kosa lolote ndani ya miezi mitatu na ataanza kutumika kwenye mechi zijazo za mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya NBC Tanzania Bara msimu uliopita.
Baada ya kurejea kutoka Ghana aliingia kwenye mgogoro mzito na uongozi na kutakiwa kufidia malipo ya pesa kwa muda wote aliozidisha baada ya kupewa ruhusa yake.

Chanzo cha habari kimeiambia Championi hapo jana kwamba, tayari Kocha Nabi kamruhusu Morrison kuungana na wenzake kwenye kikosi cha kwanza ambapo ataanza kumtumia kwenye michezo ijayo ila hatakiwi kuonyesha kosa la utovu wa nidhamu ndani ya miezi mitatu ijayo.

