Mshambuliaji kinara wa Simba, Mosses Phiri ameahidi kurejesha makali yake na kuendelea kufunga mabao baada ya kupona majeraha.

Phiri amesema ushindani wa namba umekuwa mkubwa baada ya kuongezwa wachezaji wapya lakini atapambana kurudisha nafasi yake.
Mosses; “Nina furaha nimerudi, sio kitu kizuri kwa mchezaji kukosa mechi nyingi kutokana na majeruhi lakini nimejipanga kuhakikisha narudi kwa nguvu kama nilivyoanza msimu.”

Mshambuliaji huyo kwa sasa yuko fiti na amesema kuwa baada ya mchezo dhidi ya Singida atakuwa tayari kucheza na amejipanga kuhakikisha anaendeleza ubora wake.
Akizungumzia kuhusu ujio wa mshambuliaji, Jean Baleke, Phiri amesema “Ni mchezaji mzuri, ana kasi pia anajua kufunga naamini ataisaidia timu.”

