Nyota wa zamani wa Ligi Kuu ya Uingereza Christian Atsu ambaye aliwahi kuichezea Chelsea, Newcastle na Everton amepatikana akiwa hai lakini amejeruhiwa kufuatia tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.7 nchini Uturuki. Odds kubwa za soka unazipata Meridianbet.

Winga huyo wa zamani wa Chelsea na Newcastle, ambaye sasa anakipiga katika klabu ya Super Lig ya Hatayspor, alikosekana baada ya mfululizo wa matetemeko makubwa ya ardhi ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 4,000 kote Uturuki na Syria.
Atsu alikumbwa na janga hilo la asili huko Kahramanmaras, ambapo Hatayspor wanakaa, pamoja na mkurugenzi wa michezo wa klabu Taner Savut. Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.
Makamu wa rais wa Hatayspor Mustafa Ozat sasa amethibitisha kuwa Christian Atsu ametoka kwenye vifusi lakini amejeruhiwa, huku juhudi za kumtafuta Savut zikiendelea.
Ozat alisema: “Christian Atsu alitolewa nje akiwa na majeraha. Mkurugenzi wetu wa michezo, Taner Savut, kwa bahati mbaya bado yuko chini ya vifusi.”
Aliongeza: “Hatay aliathirika sana. Tunakaribia mwisho wa saa za hatari zaidi.”
Balozi wa Ghana nchini Uturuki, Francisca Ashitey-Odunton, amepokea taarifa kutoka kwa mamlaka ya soka ya nchi hiyo kuwa Christian Atsu amepatikana. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!.
Mchezaji mwenzake wa Christian Atsu Kerim Alici, rafiki wa karibu, pia amethibitisha kwenye TV ya Uturuki kwamba mchezaji huyo ameokolewa.
Wachezaji wengine wawili kutoka Hatayspor, Burak Oksuz na Bertug Yildirim pia wameokolewa kutoka kwenye vifusi.
Mchezaji wa kimataifa wa Ghana Christian Atsu alijiunga na Chelsea mwaka 2013, ambapo alisafirishwa kwa mkopo kwenda Everton na Bournemouth, pamoja na Vitesse, Malaga na Newcastle. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa na zawadi ya ukaribisho ukijiunga. Bashiri hapa.

