Kochaa wa klabu ya Fc Barcelona Xavi Hernandez amesema nyota wa klabu hiyo Ansu Fati hayupo kwenye mipango ya kuuzwa ndani klabu hiyo na ataendelea kusalia klabuni hapo.
Siku kadhaa nyuma taarifa mbalimbali zimeeleza kua nyota Ansu Fati anataka kuuzwa na klabu hiyo na klabu ya Manchester United ikitajwa kwenye dili hilo, Lakini kocha Xavi amezima uvumi huo uliokua unaendela mitandaoni.
Wakati anaongea na waandishi wa habari mapema leo kocha huyo aliulizwa kuhusu Ansu Fati kuondoka kwenye timu hiyo na kocha huyo alijibu kwa kusema ” Ansu Fati hauzwi kama mwingine yeyote kwasasa, Sio muda wa kuongelea usajili. Namuamini Ansu Fati kwa mipango ya sasa na ya baadae na ni mchezaji wetu”
Mchezaji Ansu Fati amekua akiandamwa na majeraha ya mara kwa mara ndani ya klabu hiyo ikiwa inaelezwa ndio sababu ya klabu hiyo kufikiria kumuuza mchezaji huyo, Lakini Xavi yeye kwake anaona kama uzushi tu kwani klabu hiyo haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo.
Ansu Fati ambaye ametoka kwenye akademi ya klabu ya Barcelona na ni mchezaji ambaye alitabiriwa kufanya makubwa sana ndani ya klabu hiyo kutokana na kipaji kikubwa ambacho amekua nacho, Lakini inaonekana kama majeraha ya mara kwa mara yanaweza kuharibu kipaji chake.

