Al Nassr wamesherehekea uchezaji wa Cristiano Ronaldo ambao umevunja rekodi katika Taifa la Ureno.

Kwa kuzingatia kujitolea kwake katika soka Ronaldo anaweza kuwa hakula keki aliyokabidhiwa hapo jana.
Al Nassr walikuwa wakisherehekea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kwa wanaume wakati wote.
Ronaldo alicheza mechi yake ya 197 kwa Ureno mnamo Machi 23, akifunga mara mbili katika kichapo cha 4-0 kutoka kwa Liechtenstein.

Sambamba na kuashiria mafanikio hayo, Al Nassr pia alisherehekea miaka 25 ya kuzaliwa kwa Abdulrahman Ghareeb.
Klabu iliandika katika ukurasa wake wa Twitter; “Leo, tunasherehekea rekodi na siku ya kuzaliwa. Rekodi ya mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi katika soka ya kimataifa na siku ya kuzaliwa ya mchezaji mwenye kipawa wa Saudi.”

