Mshambuliaji wa Kagera Sugar Anuary Jabir amepata mwaliko wa wiki mbili wa kufanya majaribio na klabu ya KAA Gent ya nchini Ubelgiji inayoshiriki First Division A.

Anuary Jabir atafanya majaribio na klabu hiyo na endapo kiwango chake kiwawavutia huenda akajiunga na klabu hiyo ya Ubelgiji huku klabu yake ya Kagera Sugar ikimtakia kila lakheri kwenye majaribio hayo.
KAA Gent ipo nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi hiyo inayowakilishwa na timu 18 huku ikiwa imeshinda michezo yake 16, kwenye 31 ambayo wamecheza, sare 6 na kupoteza mara 9 hadi sasa.

Mechi ya mwisho waliyocheza walishinda kwa kishindo mabao 5-0 wakiwa ugenini. Tofauti yao na timu inayoongoza ligi ni pointi 17.
Je Anuary anaweza kufanikisha kile ambacho kitakuwa kimempeleka na Tanzania ikashuhudia vijana wake wakicheza nje ya Tanzania na vilabu vikubwa? Bashiri mechi zako na Meridianbet kwa ODDS KUBWA.

