Rasmi jana klabu ya Ruvu Shooting imeshuka daraja baada ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba SC kwenye mchezo ambao ulipigwa katika dimba la Chamazi jijini Dar es salaam.

Mpaka kufikia kipindi cha mapumziko Simba alikuwa akiongoza bao moja ambalo lilitupiwa kimyani na kiungo wao Cloutus Chama kabla ya baadae Pape Sakho kufunga mabo mawili ya kuikandamiza Ruvu Shooting.
Hata hivyo hata angepata ushindi, Ruvu asingeweza kwenda nafasi yoyte ya juu kutokana na pointi ambazo alikuwa nazo hivyo ni alikuwa akikamilisha ratiba tuu na msimu ujao atakuwa akishiriki ligi daraja la kwanza.

Baada ya kupata pointi tatu mnyama amesalia kwenye nafasi ya pili akiwa na alama zake 67 baada ya michezo 28 ambayo amecheza hadi sasa huku msimu huu ukiwa mbaya baada ya kukosa makombe yote.
Je Ruvu ataungana na nani kwenda ligi daraja la kwanza kwani kuna Polisi Tanzania ambaye anashikilia nafasi ya pili kutoka mwisho akiwa na pointi 22 pekee zikiwa zimesalia mechi tatu?

