Ten Hag: Asema Diallo Yupo Kwenye Mipango Yake

Kocha wa klabu ya Manchester United Erik Ten Hag amesema kua kinda wa klabu hiyo Amad Diallo yupo kwenye mipango na atampa nafasi kwenye timu yake baada ya kumaliza mkopo kwenye klabu ya Sunderland.

Kinsa Amad Diallo alitolewa kwa mkopo wa msimu mzima ndani ya klabu ya Sunderland na kufanikiwa kuonesha kiwango bora kabisa, Hivo kocha Ten Hag anaona kijana huyo ana uwezo kurejea kwenye timu hiyo na kupata nafasi katika msimu wa 2023/24.ten hagKocha Ten Hag amekua muumini wa vijana kwa muda mrefu hata alipokua ndani ya klabu ya Ajax alikua na mwendelezo mzuri wa kuwapa nafasi vijana wadogo kwenye timu yake na wanakuja kufanya vizuri, Ndani ya Manchester United ameonesha imani kubwa kwa kijana mdogo Alejandro Garnacho ambaye anafanya vizuri mpaka sasa.

Amad Diallo amekua na msimu bora ndani ya klabu ya Sunderland Ten Hag kusema mchezaji huyo ana nafasi ndani ya timu hiyo na walimpeleka kwa mkopo kwajili ya kukua na kocha huyo amekiri ameona maendeleo ya Amad hivo mchezaji huyo atakua sehemu ya timu msimu ujao.ten hagAmad Diallo sasa anahitajika kupambania namba ndani ya klabu hiyo msimu ujao kama anataka nafasi ya kucheza zaidi kwani nafasi anayocheza ndani ya klabu hiyo ina watu wengi, Hivo anapaswa kupambana zaidi ili aweze kumshawishi mwalimu ampe nafasi kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.