KMC Yarudisha Matumaini Kubaki Ligi Kuu Yaipasua Singida

Klabu ya KMC imefufua matumaini ya kuendelea kuwepo kwenye ligi kuu ya NBC msimu wa 2023/24 baada ya kuipasua klabu ya Singida Big Stars leo katika mchezo uliopigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar-es-salaam.

KMC wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili wa bila katika mchezo huo huku mabao ya klabu hiyo yakifungwa na Daruwesh Saliboko alioipatia klabu hiyo bao la la kwanza katika mchezo na msumari wa mwisho ukipigwa na Cliff Buyoya dakika ya 84 ya mchezo.KMCKlabu hiyo baada ya kushinda mchezo wa leo imefanikiwa kupanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufanikiwa kufikisha alama 29, Hivo wameibua matumaini upya ya kuendelea kubaki ligi kuu kwa msimu ujao chini ya kocha wao wa sasa Jamhuri Kihwelu.

Timu ya KMC pia leo itachukua shilingi milioni moja kutoka kwa wadhamini wao wakuu kampuni ya Meridianbet ambao waliahidi watanunua kila goli litakalofungwa na klabu hiyo kwa shilingi laki tano, Hivo klabu hiyo leo itachukua milioni moja kwa wadhamini hao wakuu.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.