Messi Kurejea Kesho Dhidi ya Ajaccio

Staa wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa na mchezaji bora wa dunia mara saba Lionel Messi kurejea kesho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa dhidi ya klabu ya Ajaccio hiyo ni baada ya staa huyo kukutwa na kosa la kuondoka klabuni bila ruhusa.

 

Lionel Messi alikutwa na hatia ya kuondoka klabuni hapo na kwenda nchini Saudia Arabia bila ruhusa kutoka klabuni kitendo ambacho kilimuweka kwenye wakati mgumu na kulazimika kuomba radhi hadharani kutokana na kitendo hicho wiki moja iliyomalizika.MessiKocha wa klabu ya PSG Chrisopher Galtier amesema kua nyota huyo amefanya mazoezi na klabu hiyo na yuko vizuri kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Ajaccio, Ikumbukwe mchezaji huyo alipewa adhabu ya kutokushiriki shughuli zozote za kimichezo ndani ya klabu hiyo kwa muda wa wiki mbili lakini adhabu hiyo ilitenguliwa siku ya jumatatu wiki hii.

PSG wakiwa na Lionel Messi kesho watashuka dimbani kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi ili kujiweka mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao ambao waliutwaa msimu uliomalizika hivo mchezo wa kesho ni muhimu kwa klabu hiyo kwani klabu ya Lille wanaifukuza klabu hiyo kimyakimya.MessiLicha ya kumalizana na klabu ya PSG juu ya kitendo cha utovu wa nidhamu alichokifanya Messi bado hajasaini kandarasi yeyote ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo, Kwani mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu huku taarifa zikieleza anajiandaa kurejea ndani ya klabu ya Barcelona.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.