Sergio Ramos atamfuata Lionel Messi kutoka Paris St Germain huku mabingwa hao wa Ufaransa wakithibitisha kuondoka kwa beki huyo mkongwe wa Uhispania mwishoni mwa kandarasi yake.

Ramos amekaa kwa misimu miwili iliyopita Parc des Princes baada ya kujiunga kutoka Real Madrid kwa uhamisho wa bure, lakini yuko tayari kucheza mechi yake ya mwisho hii leo dhidi ya Clermont Foot.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 ameshinda mataji mfululizo ya Ligue 1 akiwa na PSG, akifunga mabao matano katika mechi 57, ingawa kiwango chake kilitiliwa shaka mara kwa mara na kuondoka kwake hakuonekani kama jambo la kushangaza.
Ramos amesema, “Kuvaa shati Nyekundu na Bluu kwa miaka miwili iliyopita imekuwa uzoefu mzuri. Nimekuwa na tukio lisilosahaulika huko Paris na ningependa kuwashukuru nyote kwa msaada na upendo wenu. Allez Paris!”

Baadaye aliongeza kwenye Twitter: “Kesho itakuwa siku maalum, kesho nitaaga hatua nyingine ya maisha yangu, kwaheri kwa PSG.”
Rais wa klabu Nasser Al-Khelaifi alisema: Tungependa kutoa shukrani zetu nyingi kwa Sergio Ramos kwa miaka miwili ambayo amekaa nasi.

Uongozi wa Sergio, ari ya timu na taaluma, pamoja na uzoefu wake katika kiwango cha juu, vinamfanya kuwa gwiji wa soka wa kweli, na ilikuwa heshima kuwa naye Paris. Kila mtu katika klabu anamtakia kila la heri.

