Kvaratskhelia Mchezaji Bora Serie A

Winga wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Georgia Khvicha Kvaratskhelia ametangazwa kua mchezaji bora wa ligi kuu ya Italia msimu huu maarufu kama Serie A.

Kvaratskhelia amekua na msimu bora na klabu ya Napoli na kufanikiwa kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Italia baada ya muda mrefu, Huku winga huyo akiwa moja ya wachezaji mahiri zaidi ndani ya kikosi cha Napoli chini ya kocha Luciano Spaletti.KvaratskheliaWinga huyo amekua na ubora mkubwa sana akiwa amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 24 ndani ya msimu wa mwaka 2022/23 akiwa anakamata nafasi ya pili kwa wachezaji waliohusika na mabao mengi nyuma ya mchezaji mwenzake wa Napoli Victor Osimhen ambaye amehusika kwenye mabao 29.

Winga Kvaratskhelia ametangazwa kua mchezaji bora wa Serie A ikiwa sio kwa bahati mbaya bali ni kutokana na mfululizo wa kiwango maridhawa ambao amekua nacho ndani ya msimu huu uliomalizika na klabu yake ya Napoli kufanikiwa kutawazwa kua mabingwa wa Serie A baada ya miaka mingi.KvaratskheliaNapoli imefanikiwa kua na msimu bora sana ndani ya ligi kuu ya Italia na kufanikiwa kuazalisha wachezaji wengi wenye ubora na kuzivutia timu mbalimbali barani ulaya, Huku mmoja wao ni winga Kvaratskhelia ambaye ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi hiyo na kwasasa ameanza kufatiliwa kwa karibu na vilabu vikubwa barani humo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.