Real Madrid inamfukuzia Kai Havertz

Klabu ya Real Madrid inamfukuzia mchezaji wa Chelsea raia wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz katika dirisha hili kubwa majira ya joto ili kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao katika safu ya ushambuliaji.

Real Madrid inahitaji mshambuliaji mwingine ili kuboresha timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji na Kai Havertz ameingia kwenye orodha ya wababe hao wa soka nchini Hispania, Hivo klabu hiyo inafikiria kutuma ofa kwa klabu ya Chelsea kwajili ya kumpata mchezaji huyo.real madridKlabu ya Chelsea inafahamika kua ipo kwenye mazungumzo na mshambuliaji Kai Havertz juu ya kumuachia mjerumani huyo, Lakini klabu hiyo imeweka bayana itamuuza jumla na suala la kutolewa kwa mkopo sio kipaumbele chao hivo wako tayari kusikiliza ofa kwa klabu ambazo zitakua zinamtaka mchezaji huyo.

Real Madrid wao watatuma ofa kwa klabu ya Chelsea lakini inafahamika kua klabu hiyo haipo tayari kutoa dau kubwa kununua mshabuliaji sokoni katika majira haya ya joto, Kwani mchezaji pekee ambaye wamepanga kumsajili kwa gharama kubwa ni kiungo wa kimataifa wa Uingereza Jude Bellingham ambaye anakipiga klabu ya Borussia Dortmund.real madridTaarifa za mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Karim Benzema kuondoka klabuni hapo na kutimkia Saudia Arabia zimeifanya klabu hiyo kuanza kutafuta mshambuliaji mwingine haraka sokoni, Huku kipaumbele chao kikiwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani Kai Havertz.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.