Qatar Kuwasilisha Ofa ya Mwisho Man United Ijumaa Hii

Kampuni ya Qatar chini ya Sheikh Jassim Emir El Thani kuwasilisha ofa yao ya mwisho ya kuinunua klabu ya Manchester United ambapo itakua na lengo lilelile la kuichukua klabu hiyo jumla.

Kampuni ya Qatar Group imekua miongoni  mwa kampuni zilizojitokeza kwajili ya kuinunua klabu ya Manchester United wakichuana na Sir Jim Ratcliff, Lakini kampuni hiyo iko tofauti na mpinzani wake ambae ni raia wa Uingereza ambapo wao wanataka kuichukua jumla klabu hiyo.QatarSheikh Jassim anatawasilisha ofa yake ijumaa hii ambayo itakua ni ofa ya tano ambapo ofa zingine nne zilipigwa chini na wamiliki wa sasa wa klabu hiyo familia ya Glazers, Lakini kampuni hiyo ilisheleza nia yake ni kuichukua klabu hiyo kwa umiliki wa aslimia na kulipa madeni yote ambayo klabu hiyo inadaiwa.

Qatar Group wanapowasilisha ofa yao ijumaa hii wameweka wazi kua kama ofa yao hiyo ya kuichukua klabu ya Manchester United haitakubalika na wamiliki wasasa wa United Familia ya Glazers basi hawatajihusisha tena na mchakato wa kuinunua klabu hiyo tena.QatarFamilia ya Glazers walitangaza kuiweka sokoni klabu hiyo mwishoni mwa mwaka jana lakini wameonekana kua na masharti mengi ambayo Qatar Group wanaona kama vikwazo kwa upande wao,Jambo ambalo limefanya kampuni hiyo itangaze ofa ya mwisho na kama ikishindikana basi watajiondoa kwenye mchakato.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.