Baada ya kuikataa Aston Villa, Juventus sasa wanatumai kuwa Weston McKennie atakubali kuhamia Fenerbahce ambayo kwasasa itakuwa ikinolewa na Jose Mourinho.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya uhamisho wa Sportitalia Alfredo Pedullà, hali bado iko katika hatua za awali hasa kwani kiungo huyo amekataa kufikiria mustakabali wake hadi baada ya USMNT kumaliza uzoefu wake wa Copa America.
Mourinho angependa kumleta McKennie nchini Uturuki na Juventus wamekuwa wazi kuwa muda wake wa kukaa Turin umekwisha chini ya kocha mpya Thiago Motta.


