TAARIFA za uhakika ambazo Meridian Sports imezipata kutoka ndani ya Yanga ni Kwamba, kiungo wao raia wa Ivory Coast Pacome ZouaZoua ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Pacome ambaye mkataba wake ulikua unafika ukomo mishoni mwa Msimu Ujao, amefikia hatua hiyo baada ya kuona mipango mizuri ya Yanga na kuboreshewa maslahi yake.“Ni kweli tumemuongezea mkataba mpya wa kuendelea kuichezea YANGA, amepewa mkataba wa miaka miwili na kuboreshewa maslahi yake.