Baada ya kuikataa Aston Villa, Juventus sasa wanatumai kuwa Weston McKennie atakubali kuhamia Fenerbahce ambayo kwasasa itakuwa ikinolewa na Jose Mourinho.
Kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya uhamisho wa Sportitalia Alfredo Pedullà, hali bado iko katika hatua za awali hasa kwani kiungo huyo amekataa kufikiria mustakabali wake hadi baada ya USMNT kumaliza uzoefu wake wa Copa America.
Mourinho angependa kumleta McKennie nchini Uturuki na Juventus wamekuwa wazi kuwa muda wake wa kukaa Turin umekwisha chini ya kocha mpya Thiago Motta.
Mchezaji huyo wa zamani wa Leeds United atakuwa mchezaji huru Juni 2025 na hivyo Juve wanatamani sana kumuondoa kwa €15m pamoja na bonasi.
Hapo awali alikuwa katika mpango wa kubadilishana na Aston Villa kwa ajili ya Douglas Luiz, lakini alishikilia msimamo wake kwa kukataa kukubaliana na masuala binafsi na upande wa Ligi Kuu.
Badala yake, Bianconeri walimuongeza Enzo Barrenechea kwenye kifurushi na Samuel Iling-Junior na pesa taslimu.
This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.
Strictly Necessary Cookies
Strictly Necessary Cookie should be enabled at all times so that we can save your preferences for cookie settings.
If you disable this cookie, we will not be able to save your preferences. This means that every time you visit this website you will need to enable or disable cookies again.