Mabosi wa Yanga wamebainisha kuwa hakuna kipengele kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi ambao unatarajiwa kuchezwa leo Machi 8 2025, saa 1:15 Uwanja wa Mkapa.

Na Kwamba watakwenda uwanjani Kama kawaida na hakuna siku nyingine yoyote ambayo mechi hiyo itachezwa kama siyo leo kWa kuwa utaratibu wote wa mechi hiyo wao wameshafanya.
Uongozi wa Simba usiku wa kuamkia Machi 8 2025 walitoa taarifa kwamba hawatashiriki mchezo kutokana na kutopewa ruhusa ya kufanya mazoezi Uwanja wa Mkapa siku moja kabla ya mchezo.
Wakati hayo yakitokea Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara taarifa rasmi kupitia ukurasa wa Instagram imeeleza namna hii: “Ile siku imefika.” Taarifa hiyo imesindikizwa na ujumbe wa mechi ya Kariakoo Dabi ambayo inatarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa.
Taarifa zinaeleza kuwa uongozi wa Simba haupo tayari kwa mchezo wa leo na wamegomea mazima suala hilo kwa mujibu wa kanuni.


