Selemani Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Singida Black Stars ambao ni mzunguko wa pili.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Liti baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 0-1 Simba SC.
Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Fabrince Ngoma kwa pasi ya Jean Ahoua ambaye alipiga kona ya moja kwa moja iliyokutana na kichwa cha Ngoma.
Matola amesema kuwa wapinzani wao wapo imara kutokana na aina ya timu waliyonayo pamoja na kikosi bora walichonacho.


