Kipa wa Simba SC, Aishi Manula inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wa Azam FC ambao wanahitaji saini yake.

Ipo wazi kwamba Manula kwa msimu wa 2024/25 hajawa chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu,Fadlu Davids.
Katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara hajaanza langoni mchezo hata mmoja na kwenye anga la kimataifa pia jina lake lilikuwa linaondolewa kwenye siku za safari.
Kwenye mechi zote za fainali ugenini na Tanzania, dhidi ya RS Berkane ni Moussa Camara, kipa namba moja wa Simba SC alianza na benchi alikuwa Ally Salim.
Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Azam FC wanahitaji saini ya kipa huyo ambaye ni miongoni mwa wazawa wenye uwezo mkubwa awapo langoni.


