Kamishna wa Michezo Zanzibar Ameir Mohammed amekanusha vikali juu ya taarifa za maatundu yaliyosambaa mitandaoni kuwa kulikuwa na vitendo vya kishirikina katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo wa Dabi kati ya Simba SC na Yanga SC uliochezwa katika uwanja wa New Amaan Complex Machi 1 mwaka huu.

Ameir amesema taarifa hizo si za kweli na zimepotosha umma kuhusu mazingira halisi ya vyumba hivyo vilivyotumiwa na timu hizo wakati wa mchezo huo mkubwa uliochezwa Zanzibar.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akifafanua kuhusu matundu yaliyoonekana kwenye kuta za vyumba vya kubadilishia nguo, amesema hayakuwekwa kwa ajili ya kuweka dawa kama ilivyodaiwa, bali yalikuwa ni sehemu maalum zilizotumika kupitisha nyaya za kamera za ulinzi (CCTV) zilizowahi kuwekwa uwanjani hapo.

Ameongeza kuwa matundu hayo yalikuwepo katika vyumba vya timu zote mbili, Simba na Yanga, na kueleza kuwa kamera hizo ziliwahi kuondolewa baada ya CAF kuagiza zisitumike ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mashindano ya CHAN kwa sababu za kulinda faragha ya wachezaji na timu.
Kuhusu matundu yaliyoonekana katika njia wanazopita wachezaji kuelekea uwanjani, Ameir amesema maeneo hayo yalikuwa sehemu za kufungwa mabango ya matangazo ya wadhamini mbalimbali, ikiwemo kampuni ya TotalEnergies.

Aidha, ameeleza kuwa kupauka kwa baadhi ya maeneo ya nyasi uwanjani kulitokana na maji yaliyomwagwa kwa imani za kishirikina, huku akilitaka Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) kuchukua hatua stahiki baada ya mlango mmoja wa uwanja kuvunjwa, akisisitiza kuwa timu husika inapaswa kuwajibishwa kwa uharibifu huo.

