Ratiba ya Hatua ya 16 Bora Kombe la CRDB Yatangazwa

Ratiba ya michezo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB imetangazwa mara baada ya kumalizika kwa michezo ya hatua ya 32 bora, huku timu mbalimbali zikifuzu na kuendelea na hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Ratiba ya Hatua ya 16 Bora Kombe la CRDB Yatangazwa

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mabingwa watetezi Yanga SC watakutana na TMA Stars katika mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Wakati huo huo wapinzani wao wa jadi Simba SC wao watacheza dhidi ya Dodoma Jiji FC katika hatua hiyo ya 16 bora.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika michezo mingine, Singida Big Stars watamenyana na Mbeya City FC, huku Azam FC wakitarajiwa kuvaana na Fountain Gate FC katika pambano lingine la kusisimua.
Pia Namungo FC wao watakipiga dhidi ya TRA FC, wakati Coastal Union wakikabiliana na Pamba Jiji FC.

Ratiba ya Hatua ya 16 Bora Kombe la CRDB YatangazwaKatika mechi nyingine za hatua hiyo, JKT Tanzania watamenyana na Mbuni FC, huku Geita Gold FC wakicheza dhidi ya Mashujaa FC kumalizia ratiba ya michezo ya hatua ya 16 bora.
Mashindano ya Kombe la Shirikisho la CRDB yanaendelea kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, huku timu zikilenga kusonga mbele hadi hatua za mwisho za mashindano hayo ambayo mshindi wake hupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa barani Afrika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.