Michuano ya Kombe la shirikisho la CRDB inaendelea katika hatua ya 32 bora ambapo klabu ya Simba SC leo itashuka dimbani kuikabili B19 FC maarufu kama Mababeru wa Jiji. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Meja General Isamuyo jijini Dar es Salaam majira ya saa 1:15 usiku.

Simba inaingia katika mchezo huo ikiwa na changamoto ya kuwakosa baadhi ya nyota wake muhimu wa safu nya ushambuliaji. Miongoni mwa wachezaji watakaokosekana ni mshambuliaji Selemani Mwalimu ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu, pamoja na Jonathan Sowah ambaye anakabiliwa na changamoto za kinidhamu ndani ya klabu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Katika michezo mingine ya hatua hiyo iliyochezwa jana Machi 6, klabu ya TRA united fc iliibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Kijiwe Nongwa FC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Black Rhino Academy mkoani Arusha.
Pia klabu ya Dodoma Jiji FC ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Sports ya Tanga katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Katika mchezo mwingine uliopigwa jijini Dar es Salaam, JKT Tanzania iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hausung FC kwenye Uwanja wa Meja General Isamuyo.
Hatua ya 32 bora itaendelea kesho jumapili Machi 8 kwa michezo mingine mikubwa ambapo Yanga SC itamenyana na Polisi Tanzania fc katika Uwanja wa KMC Complex saa 1:15 usiku, huku Azam FC ikitarajiwa kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza FC katika Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 1:15 usiku.


