Klabu ya Bayern Munich imeendelea kuimarisha harakati zake za kutwaa ubingwa wa Bundesliga baada ya kuifunga Borussia Mönchengladbach mabao 4-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena.

Bayern ilianza mchezo huo kwa kasi na mapema ilipata bao ambalo lilifutwa kutokana na kuotea baada ya Lennart Karl kuonekana ameotea. Hata hivyo shinikizo la wenyeji liliendelea hadi walipopata bao la kwanza kupitia Luis Díaz aliyefunga kwa shuti la kuvutia kufuatia pasi ya Leon Goretzka.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Bao la pili lilipatikana mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya Konrad Laimer kufunga kwa shuti kali kufuatia maandalizi mazuri ya Diaz. Wakati huo huo mshambuliaji Nicolas Jackson ambaye alikuwa akichukua nafasi ya Harry Kane alionyesha kiwango kizuri katika safu ya ushambuliaji.
Katika kipindi cha pili, mambo yalizidi kuwa magumu kwa Gladbach baada ya Rocco Reitz kupewa kadi nyekundu kwa kumwangusha Jackson akiwa katika nafasi ya kufunga. Baada ya tukio hilo, Jamal Musiala alifunga bao la tatu kwa mkwaju wa penalti na kuweka Bayern mbele zaidi.

Bayern iliendelea kutawala mchezo huo na baadaye kupata bao la nne kupitia Nicolas Jackson aliyemalizia mpira uliotengenezwa na Karl. Katika mchezo huo pia chipukizi wa miaka 17 Maycon Cardozo alifanya debut yake kwa mara ya kwanza.
Gladbach walipata bao lao la kufutia machozi mwishoni mwa mchezo kupitia Wael Mohya ambaye aliweka rekodi ya kuwa mfungaji mdogo zaidi wa klabu hiyo katika Bundesliga. Ushindi huo unaifanya Bayern kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 14, huku wakijiandaa na mchezo wao ujao wa UEFA Champions League dhidi ya Atalanta BC.


