Baada ya siku chache tangu Yanga na Simba kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara uliomalizika kwa sare kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, timu hizo zimeorodheshwa kati ya nane zinazotarajiwa kushiriki Kombe la Muungano 2026. Kushiriki kwake kunamaanisha Yanga na Simba zitarudi Zanzibar kujaribu kudumisha heshima baada ya kushindwa kutambiana Machi 1, 2026.

Kabla ya hayo, Yanga ilishuhudia mafanikio makubwa kwa kubeba Kombe la Mapinduzi 2026, baada ya kuifunga Azam katika fainali iliyochezwa Januari 13, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba. Simba na Yanga ni miongoni mwa timu nne za Tanzania Bara zitakazoshiriki mashindano hayo kuanzia Aprili 21 hadi 26, 2026, huku zingine zikiwa Singida Black Stars na Azam FC.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Simba na Singida Black Stars walishia nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2026, zote zikipoteza kwa 1-0 dhidi ya wapinzani wao, huku Yanga ikibeba ubingwa. Kwa upande wa Zanzibar, michuano itawakilishwa na Mlandege FC, Muembe Makumbi City, Mafunzo, na KVZ.

Yanga ni bingwa mtetezi wa Kombe la Muungano, baada ya kulibeba mwaka jana 2025 kwa kuifunga JKU FC 1-0 katika fainali iliyochezwa Mei 1, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba. Ushindi huo umewafanya Yanga kuwa kinara wa Kombe hilo, mara saba.

Mashindano ya Kombe la Muungano 2026 yatarajiwa kutoa fursa kwa timu zote kushindana kwa ubora wa juu kwa ajili ya vikosi hivyo kujiweka sawa saw ana kutoa fursa kwa wachezaji ambao wamekuwa hawana nafasi kwenye vilabu hivyo ili kuonyesha uwezo wa.

