Arne Slot: Uzoefu wa Mchezo wa Awali Utasaidia Liverpool Dhidi ya Galatasaray

Kocha wa Liverpool FC, Arne Slot, amesema mchezo wao wa awamu ya 16 bora ya UEFA Champions League dhidi ya Galatasaray utawasaidia kushughulikia hali ya presha ya mashabiki uwanjani katika mchezo wa leo, baada ya kukukutana na hali hiyo mapema msimu huu mjini Istanbul.

Arne Slot: Uzoefu wa Mchezo wa Awali Utasaidia Liverpool Dhidi ya Galatasaray
Liverpool waliikubali kichapo kutoka kwa Galatasaray 1-0 kwenye hatua ya makundi mwezi Septemba katika Uwanja wa Rams Park, tukio lililoacha alama kwa wachezaji kutokana na kelele kubwa za mashabiki wa nyumbani.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Slot amesema klabu hiyo ya Uturuki ina mashabiki wenye shauku kubwa na mara nyingi hufanya mashabiki wa timu za wageni kuhisi woga, kama ilivyokuwa Manchester United walipokaribishwa na bango lenye maneno “welcome to hell” kabla ya mchezo wa Kombe la Ulaya mwaka 1993.

Arne Slot: Uzoefu wa Mchezo wa Awali Utasaidia Liverpool Dhidi ya Galatasaray

Slot amesema kila mchezaji wa Liverpool anatarajia kukabiliana na shinikizo siyo tu kutoka kwa mashabiki bali pia na wachezaji 11 wenye ujuzi na kocha bora, Slot akibainisha kuwa uzoefu wa awali wa kelele hizo uwanjani ni chachu chanya kwa timu yake.

Mchezo huu wa mkondo wa kwanza uwanjani Galatasaray unaashiria mechi ya 100 ya Slot kama kocha wa Liverpool, ambapo atajaribu kuvunja rekodi ya Kenny Dalglish ya idadi ya ushindi katika mechi 100 za mwanzo ikiwa ataweza kuongoza Reds kushinda uwanjani mara ya kwanza dhidi ya Galatasaray.

Arne Slot: Uzoefu wa Mchezo wa Awali Utasaidia Liverpool Dhidi ya Galatasaray

Liverpool itashuka dimbani usiku wa leo majira ya saa 2:45 huku akiwakosa wachezaji wake muhimu wanaounda kikosi cha kwanza kipa namba moja Alisson Becker mwenye majeraha Pamoja na Federico Chiesa

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.