Klabu ya Chelsea inaendelea kuwa na matumaini kuwa kiungo wao Enzo Fernández atasalia ndani ya kikosi hicho msimu huu wa kiangazi, licha ya kuvutiwa na vilabu vikubwa barani Ulaya ikiwemo Real Madrid, Paris Saint-Germain na Manchester City.
Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya klabu hiyo, kuna mashaka iwapo klabu hizo zitaweza kuwasilisha ofa itakayokidhi thamani inayohitajika na Chelsea. Kiungo huyo alinunuliwa kwa ada ya pauni milioni 106.8, hivyo klabu hiyo inasisitiza kuwa haitazingatia kuuza kwa kiwango cha chini ya hapo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Bei ndiyo kikwazo kikubwa kwa sasa, na ndani ya klabu hakuna matarajio makubwa kwamba kuna timu itakayofikia kiwango hicho,” kilieleza chanzo kimoja cha karibu na maamuzi ya klabu.
Aidha, uongozi wa Chelsea unaonekana kuwa na msimamo wa kuepuka mabadiliko makubwa ya kikosi katika dirisha lijalo, wakiamini kuwa kufanya hivyo kunaweza kudhoofisha utulivu wa timu ambayo tayari imepitia msimu mgumu.
“Tunataka kulinda msingi wa kikosi hiki ili kujenga timu imara zaidi kwa siku zijazo,” kiliongeza chanzo hicho, kikisisitiza umuhimu wa kumbakiza Fernandez kama sehemu ya mipango ya muda mrefu.
Mabadiliko ya benchi la ufundi pia yamechangia kuongeza matumaini ya kumbakiza mchezaji huyo, kufuatia kuondoka kwa kocha Liam Rosenior ambapo klabu sasa inatafuta kocha mwenye uzoefu na uwezo wa kurejesha makali ya timu.
“Tunahitaji sauti mpya yenye mamlaka na maono ya wazi, ambayo inaweza kumrejesha Fernandez katika kiwango chake bora,” kilisema chanzo hicho, kikiongeza kuwa kocha mpya anaweza kuwa chachu ya mabadiliko chanya ndani ya kikosi.
Hata hivyo, pamoja na nia ya Chelsea kumbakiza, ushindani kutoka kwa vilabu vikubwa bado upo, huku uwezekano wa kuondoka kwa mchezaji huyo ukitegemea zaidi kupatikana kwa ofa kubwa sana. Chelsea pia inapanga kumpa mkataba mpya ili kuimarisha ushirikiano wake na kiungo mwenzake Moisés Caicedo kama sehemu ya mkakati wa kurejesha mafanikio ya timu.

