Aliyekuwa kocha wa CR Flamengo, Felipe Luis, anaripotiwa kuwa miongoni mwa makocha wanaowania kuchukua nafasi ya ukocha katika Chelsea FC kufuatia kufutwa kazi kwake mapema mwezi Machi.
Luis mwenye umri wa miaka 40 alikuwa na kipindi cha mafanikio ndani ya Flamengo, akifanikiwa kushinda ubingwa wa ligi pamoja na taji la Copa Libertadores katika muda wake wa takribani mwaka mmoja na nusu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Pamoja na mafanikio hayo, alifutwa kazi kwa kushangaza baada ya ushindi mkubwa wa mabao 8-0 dhidi ya Madureira RJ, huku ripoti zikidai kuwa sababu mojawapo ni mazungumzo aliyokuwa nayo na kampuni ya uwekezaji ya BlueCo inayohusishwa na Chelsea.
“Ilikuwa ni hali ya kushangaza sana. Nilidhani mazungumzo yalikuwa kwa nafasi kubwa zaidi, lakini baadaye nikagundua haikuwa hivyo,” alinukuliwa Luis akielezea hali hiyo.
Inaelezwa kuwa awali Luis aliamini kuwa alikuwa akizungumza kuhusu nafasi ya kuchukua mikoba ya Enzo Maresca, lakini baadaye akagundua mazungumzo hayo yalihusiana na klabu ya Strasbourg, jambo lililomfanya ajiondoe kwenye mchakato huo.


