Kipa wa Manchester City, James Trafford, amesema kurejea kwake klabuni hapo msimu huu kumekuwa na changamoto baada ya kupata muda mchache wa kucheza kutokana na ushindani mkubwa wa nafasi ya ulinzi wa lango.
Trafford, ambaye ni zao la akademi ya City, alifanya vizuri akiwa na Burnley msimu uliopita, akifanikiwa kuweka clean sheets 29 katika mechi 45 za Championship kabla ya kurejea City mwezi Julai.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Alianza mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu, lakini baadaye nafasi yake ikapungua kufuatia ujio wa kipa wa Italia Gianluigi Donnarumma aliyejiunga siku ya mwisho ya dirisha la usajili.
“Kumekuwa na msimu wa kupanda na kushuka kwa sababu sijacheza sana. Kulikuwa na uamuzi wa kufanya majira ya joto, na kwa sasa haijawa matokeo bora zaidi, lakini nimekuwa nikijaribu kuboresha kila siku na kubaki na mtazamo chanya,” alisema Trafford
Licha ya muda mdogo wa kucheza, Trafford alipata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya England kwa mara ya kwanza mwezi Machi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Uruguay, na ana matumaini ya kuingia kwenye kikosi cha kocha Thomas Tuchel kwa ajili ya Kombe la Dunia.
“Nataka sana kuwa sehemu ya kikosi. Itakuwa uzoefu mkubwa kwangu na kitu cha ajabu, lakini kwa sasa siwezi kufanya zaidi ya kuendelea kujituma hadi wakati huo ufike,” aliongeza.
Manchester City wanatarajiwa kucheza dhidi ya Southampton katika nusu fainali ya FA Cup mwishoni mwa wiki, mechi ambayo inaweza kuendelea kumpunguzia Trafford nafasi ya kuanza.

