Shirikisho la soka Afrika, limetoa orodha ya Makocha ambao hawaruhusuwi kukaa kwenye bench la timu zao, kutokana na kukosa vigezo vya CAF A au UEFA PRO LICENCE huku Didier Gomes wa Simba akikosa vigezo hivyo kwa kuwa yeye ana (UEFA A Diploma).

Kocha mkuu wa klabu ya Simba Didier Gomes hataruhusiwa kukaa kwenye bechi la ufundi la Simba kwenye mechi za klabu bingwa Afrika (Caf Champion League) kutokana kuwa na leseni ya Uefa A Diploma huku CAF wakitaka Leseni A ya CAF au Uefa Pro kwa kocha mkuu.
Pia wakati kocha Gomes atakaa jukwaani pia kocha msaidizi wa klabu hiyo Seleman Matola mwenye leseni C naye atakaa jukwaani kwa mechi za awali kutokana na kutomaliza masomo ya leseni B ambayo inatakiwa kuwa nayo kwa kocha msaidizi.
Katika orodha hiyo pia wametajwa makocha kadhaa ambao hawaruhusiwi kukaa benchi sababu kukosa vigezo vya CAF A na UEFA Pro Licence.
Erradi Mohamed Adil • 🇷🇼 APR
Bosa Wasswa • 🇺🇬 Express FC
Diego Garzitto • 🇸🇩 El Merreich SC
Comlan Mathias • 🇧🇯 ESAE FC
Pascal Lafleurial • 🇨🇫 DFCB
Roque Sapir • 🇦🇴 GD Sagrada Esperança
Ame Khamis • 🇹🇿 KMKM
Abalo Jean-Paul 🇹🇬 ASKO
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


