Ni dhahiri kuwa sasa ni masaa machache yamesalia kabla ulimwengu haumjamshuhudia Cristiano Ronaldo akirejea Old Trafford baada ya miaka 12.
CR7 amerejea United akitoka Juventus kwa dau la £12.8M, kurejea kwa nyota huyu wa dunia, ni miongoni mwa taarifa zilizoutawala ulimwengu wa soka kwa muda sasa. Hatimaye, siku ya ulimwengu kumuona Cristiano Ronaldo ndani ya Manchester United imewadia!

Akizungumza na idara ya habari ya Man United, CR7 amenukuliwa akisema
Nina uwezo. Nipo tayari. Ndio sababu nipo hapa. Sipo kwenye mapumziko. Wakati ule ulikua ni mzuri, tulishinda mataji, nilivaa jezi hii miaka mingi iliyopita, lakini nipo hapa kushinda tena.
Manchester United itawaalika Newcastle United jumamosi hii katika dimba la Old Trafford. Hakika, ulimwengu upo makini kushuhudia mapokezi ya CR7 na nini atakachokifanya ndani ya United.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.


